1 Mambo ya Nyakati - Sura ya 1

1 Mambo ya Nyakati - Sura ya 1

1Adamu, na Sethi, na Enoshi;

2na Kenani, na Mahalaleli, na Yaredi;

3na Henoko, na Methusela, na Lameki;

4na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi.

5Wana wa Yafethi; Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi.

6Na wana wa Gomeri; Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.

7Na wana wa Yavani; Elisha, na Tarshishi, na Kitimu, na Warodani.

8Wana wa Hamu; Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.

9Na wana wa Kushi; Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama; Sheba, na Dedani.

10Kushi naye akamzaa Nimrodi; yeye akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.

11Na Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi,

12na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori.

13Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi;

14na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi;

15na Mhivi, na Mwarki, na Msini;

16na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi.

17Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi.

18Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi.

19Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani.

20Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera;

21na Hadoramu, na Uzali, na Dikla;

22na Obali, na Abimaeli, na Sheba;

23na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani.

24Shemu, na Arfaksadi, na Sala;

25na Eberi, na Pelegi, na Reu;

26na Serugi, na Nahori, na Tera;

27na Abramu, naye ndiye Ibrahimu.

28Wana wa Ibrahimu; Isaka, na Ishmaeli.

29Hivi ndivyo vizazi vyao; mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Nebayothi; kisha Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu;

30na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema;

31na Yeturi, na, Nafishi, na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.

32Na wana wa Ketura, suria yake Ibrahimu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani.

33Na wana wa Midiani; Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa. Hao wote ndio wana wa Ketura.

34Na Ibrahimu naye akamzaa Isaka. Wana wa Isaka; Esau, na Israeli.

35Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora.

36Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki.

37Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza.

38Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani.

39Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni umbu lake Lotani.

40Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana.

41Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani.

42Wana wa Eseri; Bilhani, na Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani; Usi, na Arani.

43Basi hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla hajamiliki mfalme awaye yote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba.

44Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akamiliki badala yake.

45Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akamiliki badala yake.

46Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akamiliki badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi.

47Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akamiliki badala yake.

48Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akamiliki badala yake.

49Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akamiliki badala yake.

50Baal-Hanani akafa, naye Hadadi akamiliki badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu.

51Akafa Hadadi. Na hawa ndio majumbe wa Edomu; jumbe Timna, na jumbe Alva, na jumbe Yethethi;

52na jumbe Oholibama, na jumbe Ela, na jumbe Pinoni;

53na jumbe Kenazi, na jumbe Temani, na jumbe Mibsari;

54na jumbe Magdieli, na jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu.