1 Mambo ya Nyakati - Sura ya 2

1 Mambo ya Nyakati - Sura ya 2

1Hawa ndio wana wa Israeli; Reubeni, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni;

2na Dani, na Yusufu, na Benyamini, na Naftali, na Gadi, na Asheri.

3Wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela; ambao hao watatu alizaliwa na binti Shua, Mkanaani. Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa Bwana; naye akamwua.

4Na Tamari, mkwewe, akamzalia Peresi, na Zera. Wana wote wa Yuda ni watano.

5Wana wa Peresi; Hesroni, na Hamuli.

6Na wana wa Zera; Zabdi, na Ethani, na Hemani, na Kalkoli, na Darda; hao wote ni watano.

7Na wana wa Karmi; Akani, yule mwenye kutaabisha Israeli, aliyekosa katika kitu kilichowekwa wakfu.

8Na wana wa Ethani; Azaria.

9Tena wana wa Hesroni aliozaliwa; Yerameeli, na Ramu, na Kalebu.

10Na Ramu akamzaa Aminadabu; na Aminadabu akamzaa Nashoni, mkuu wa wana wa Yuda;

11na Nashoni akamzaa Salmoni; na Salmoni akamzaa Boazi;

12na Boazi akamzaa Obedi; na Obedi akamzaa Yese;

13na Yese akamzaa Eliabu, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Abinadabu, na wa tatu Shama;

14na wa nne Nethaneli, na wa tano Radai;

15na wa sita Ozemu, na wa saba Daudi;

16na maumbu yao ni Seruya, na Abigaili. Na wana wa Seruya walikuwa, Abishai, na Yoabu, na Asaheli; hao watatu.

17Na Abigaili akamzaa Amasa; na babaye Amasa ni Yetheri, Mwishmaeli.

18Basi Kalebu, mwana wa Hesroni, akazaliwa wana na mkewe Azubu, na Yeriothi, na hawa ndio wanawe wa kiume; Yesheri, na Shobabu, na Ardoni.

19Akafa Azuba, naye Kalebu akamtwaa Efrathi, aliyemzalia Huri.

20Naye Huri akamzaa Uri; na Uri akamzaa Besaleli.

21Na baadaye Hesroni akamwingilia binti wa Makiri, babaye Gileadi; ambaye alimtwaa alipokuwa mwenye miaka sitini; naye akamzalia Segubu.

22Na Segubu akamzaa Yairi, aliyekuwa mwenye miji ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi.

23Na Geshuri na Aramu wakawapokonya miji ya Yairi, pamoja na Kenathi na miji yake, jumla yote miji sitini. Hao wote ni wana wa Makiri, babaye Gileadi.

24Tena, baada ya kufa kwake Hesroni huko Kalebu-Efrata, ndipo Abia, mkewe Hesroni, alipomzalia Ashuri, babaye Teboa.

25Na wana wa Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, walikuwa Ramu, mzaliwa wa kwanza, na Buna, na Oreni, na Ozemu; kwa Ahiya.

26Naye Yerameeli alikuwa na mke mwingine, jina lake Atara; yeye alikuwa mamaye Onamu.

27Na wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, na Yamini, na Ekeri.

28Na wana wa Onamu walikuwa Shamai, na Yada; na wana wa Shamai; Nadabu, na Abishuri.

29Na mkewe Abishuri aliitwa jina lake Abihaili; naye akamzalia Abani, na Molidi.

30Na wana wa Nadabu; Seledi, na Apaimu; walakini Seledi alikufa hana watoto.

31Na wana wa Apaimu; Ishi. Na wana wa Ishi; Sheshani. Na wana wa Sheshani; Alai.

32Na wana wa Yada, nduguye Shamai; Yetheri, na Yonathani; naye Yetheri akafa hana watoto.

33Na wana wa Yonathani; Pelethi, na Zaza. Hao ndio wana wa Yerameeli.

34Basi huyo Sheshani alikuwa hana wana wa kiume, ila binti. Naye Sheshani alikuwa na mtumwa, Mmisri, jina lake akiitwa Yarha.

35Basi akamwoza binti yake aolewe na Yarha, mtumwa wake; naye akamzalia Atai.

36Na Atai akamzaa Nathani; na Nathani akamzaa Zabadi;

37na Zabadi akamzaa Eflali; na Eflali akamzaa Obedi;

38na Obedi akamzaa Yehu; na Yehu akamzaa Azaria;

39na Azaria akamzaa Helesi; na Helesi akamzaa Eleasa

40na Eleasa akamzaa Sismai; na Sismai akamzaa Shalumu;

41na Shalumu akamzaa Yekamia; na Yekamia akamzaa Elishama.

42Na wana wa Kalebu, nduguye Yerameeli, walikuwa Mesha, mzaliwa wake wa kwanza, aliyekuwa babaye Zifu; na wana wa Maresha, babaye Hebroni.

43Na wana wa Hebroni; Kora, na Tapua, na Rekemu, na Shema.

44Naye Shema akamzaa Rahamu, babaye Yorkeamu; na Rekemu akamzaa Shamai.

45Na mwana wake Shamai alikuwa Maoni; na Maoni alikuwa babaye Bethsuri.

46Naye Efa, suria yake Kalebu, alimzaa Harani, na Mosa, na Gazezi; naye Harani akamzaa Gazezi.

47Na wana wa Yadai; Regemu, na Yothamu, na Geshani, na Peleti, na Efa, na Shaafu.

48Naye Maaka, suria yake Kalebu, akamzalia Sheberi, na Tirhana.

49Tena akamzaa Shaafu, babaye Madmana; na Sheva babaye Makbena; na babaye Gibea; naye binti Kalebu alikuwa Aksa.

50Hao walikuwa wana wa Kalebu. Wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi; Shobali, babaye Kiriath-Yearimu;

51Salma, babaye Bethlehemu; na Harefu, babaye Beth-gaderi.

52Naye Shobali, babaye Kiriath-Yearimu, alikuwa na wana; Haroe, na nusu ya Wamenuhothi.

53Na jamaa za Kiriath-Yearimu; Waithri, na Waputhi, na Washumathi, na Wamishrai; katika hao walitoka Wasorathi, na Waeshtaoli.

54Na wana wa Salma; Bethlehemu, na Wanetofathi, Atroth-beth-Yoabu, na nusu ya Wamenuhothi, na Wazori.

55Na jamaa za waandishi waliokaa Yabesi; Watirathi, na Washimeathi, na Wasukathi. Hao ndio Wakeni, waliotoka kwake Hamathi, babaye mbari ya Rekabu.