1 Mambo ya Nyakati - Sura ya 23

1 Mambo ya Nyakati - Sura ya 23

1Basi Daudi alikuwa mzee, ameshiba siku; akamtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme juu ya Israeli.

2Akawakusanya wakuu wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi.

3Nao wakahesabiwa Walawi wenye miaka thelathini na zaidi; na jumla yao kwa vichwa, mtu kwa mtu, ikapata thelathini na nane elfu.

4Katika hao ishirini na nne elfu walikuwa wa kusimamia kazi ya nyumba ya Bwana; na sita elfu walikuwa maakida na makadhi;

5na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsifu Bwana kwa vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia.

6Basi Daudi akawagawanya kuwa zamu zao sawasawa na wana wa Lawi; Gershoni, Kohathi, na Merari.

7Wa Wagershoni; Ladani, na Shimei.

8Wana wa Ladani; Yehieli mkuu wao, na Zethamu, na Yoeli, watu watatu.

9Wana wa Shimei; Shelomothi, na Hazieli, na Harani, watatu. Hao walikuwa vichwa vya mbari za baba za Ladani.

10Na wana wa Shimei; Yahathi, na Zina, na Yeushi, na Beria. Hao wanne walikuwa wana wa Shimei.

11Naye Yahathi alikuwa mkubwa wao, na Zina alikuwa wa pili; lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; basi wakawa mbari ya baba kwa kuhesabiwa pamoja.

12Wana wa Kohathi; Amramu, Ishari, Hebroni, na Uzieli, watu wanne.

13Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za Bwana, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele.

14Lakini kwa habari za Musa, mtu wa Mungu, wanawe hutajwa miongoni mwa kabila ya Lawi.

15Wana wa Musa; Gershomu na Eliezeri.

16Wana wa Gershomu; Shebueli mkuu wao.

17Na wana wa Eliezeri; Rehabia mkuu wao. Yeye Eliezeri hakuwa na wana wengine; lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.

18Wana wa Ishari; Shelomithi mkuu wao.

19Wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.

20Wana wa Uzieli; Mika mkuu wao, na Ishia wa pili.

21Wana wa Merari; Mali na Mushi. Wana wa Mali; Eleazari, na Kishi.

22Akafa Eleazari, wala hakuwa na wana, ila binti tu; na ndugu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.

23Wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi, watu watatu.

24Hao walikuwa wana wa Lawi, kwa kufuata mbari za baba zao, yaani, vichwa vya mbari za baba zao waliohesabiwa, kwa hiyo hesabu ya majina yao kwa vichwa, hao walioifanya kazi ya utumishi wa nyumba ya Bwana, wenye miaka ishirini na zaidi.

25Kwa kuwa Daudi alisema, Bwana, Mungu wa Israeli, amewastarehesha watu wake; naye hukaa Yerusalemu milele;

26wala Walawi hawahitaji tena kuichukua maskani, na vyombo vyake vyote kwa utumishi wake.

27Maana kwa maneno ya mwisho ya Daudi, hao wana wa Lawi walihesabiwa, wenye miaka ishirini na zaidi.

28Kwani kazi yao ilikuwa kuwangojea wana wa Haruni katika utumishi wa nyumba ya Bwana, nyuani, na vyumbani, na kwa kuvisafisha vitakatifu vyote, ndiyo kazi ya utumishi wa nyumba ya Mungu;

29tena kazi ya mikate ya wonyesho, na ya unga mwembamba wa sadaka ya unga; ikiwa ni wa maandazi yasiyochachwa, au wa yale yaliyotokoswa, au wa yale yaliyookwa; na kazi ya kila namna ya kipimo na cheo;

30nao wasimame kila asubuhi kumshukuru na kumsifu Bwana, na jioni vivyo hivyo;

31na kumtolea Bwana sadaka zote za kuteketezwa, katika siku za sabato, za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoagizwa, kwa hesabu kadiri ya agizo lake, daima mbele za Bwana;

32tena walinde ulinzi wa hema ya kukutania, na ulinzi wa patakatifu, na ulinzi wa wana wa Haruni, ndugu zao, katika utumishi wa nyumba ya Bwana.