1 Mambo ya Nyakati - Sura ya 24

1 Mambo ya Nyakati - Sura ya 24

1Na zamu za wana wa Haruni ni hizi. Wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.

2Lakini hao Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, wala hawakuwa na watoto; kwa hiyo Eleazari na Ithamari wakafanya ukuhani.

3Akawagawanya Daudi, na Sadoki wa wana wa Eleazari, na Ahimeleki wa wana wa Ithamari, katika utumishi kwa kadiri ya usimamizi wao.

4Wakaonekana wakuu wengi wa wana wa Eleazari kuliko wa wana wa Ithamari; wakagawanyika hivi; wa wana wa Eleazari kulikuwa na kumi na sita, waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao; na wa wana wa Ithamari, sawasawa na mbari za baba zao, wanane.

5Ndivyo walivyogawanyika kwa kura, wao kwa wao; kwani kulikuwa na wakuu wa patakatifu, na wakuu wa Mungu, wa wana wa Eleazari, na wa wana wa Ithamari pia.

6Naye Shemaya, mwana wa Nethaneli, mwandishi, aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme, na mbele ya wakuu, na Sadoki kuhani, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari, na wakuu wa mbari za baba za makuhani, na za Walawi; ikatwaliwa ya Eleazari mbari moja ya baba, na moja ikatwaliwa ya Ithamari.

7Kura ya kwanza ikamtokea Yehoiaribu, na ya pili Yedaya;

8ya tatu Harimu, ya nne Seorimu;

9ya tano Malkia, ya sita Miyamini;

10ya saba Hakosi, ya nane Abia;

11ya kenda Yeshua, ya kumi Shekania;

12ya kumi na moja Eliashibu, ya kumi na mbili Yakimu;

13ya kumi na tatu Hupa, ya kumi na nne Yeshebeabu;

14ya kumi na tano Bilga, ya kumi na sita Imeri;

15ya kumi na saba Heziri, ya kumi na nane Hapisesi;

16ya kumi na kenda Pethahia, ya ishirini Ezekieli;

17ya ishirini na moja Yakini, ya ishirini na mbili Gamuli;

18ya ishirini na tatu Delaya, ya ishirini na nne Maazia.

19Huu ndio usimamizi wao katika huduma yao, waingie nyumbani mwa Bwana kwa kadiri ya agizo lao, kwa mkono wa Haruni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyomwamuru.

20Na wa wana wa Lawi, waliosalia; wa wana wa Amramu, Shebueli; wa wana wa Shebueli, Yedeya.

21Wa Rehabia; wa wana wa Rehabia, Ishia mkuu wao.

22Wa Waishari, Shelomothi; wa wana wa Shelomothi, Yahathi.

23Na wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, Yekameamu wa nne.

24Wana wa Uzieli, Mika; wa wana wa Mika, Shamiri.

25Nduguye Mika, Ishia; wa wana wa Ishia, Zekaria.

26Wana wa Merari; Mali na Mushi; wana wa Yaazia; Beno.

27Wana wa Merari; wa Yaazia; Beno, na Shohamu, na Zakuri, na Ibri.

28Wa Mali; Eleazari, asiyekuwa na wana.

29Wa Kishi; wana wa Kishi; Yerameeli.

30Na wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi. Hao ndio wana wa Walawi, kwa kufuata mbari za baba zao.

31Hao nao wakatupiwa kura vile vile, kama ndugu zao wana wa Haruni, machoni pa Daudi mfalme, na Sadoki, na Ahimeleki, na wakuu wa mbari za baba za makuhani na za Walawi; mbari za baba za mkuu, vile vile kama za nduguye mdogo.