1 Mambo ya Nyakati - Sura ya 8

1 Mambo ya Nyakati - Sura ya 8

1Naye Benyamini akamzaa Bela, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Ashbeli, na wa tatu Ahiramu;

2na wa nne Noha, na wa tano Rafa.

3Na Bela alikuwa na wana; Adari, na Gera, na Abihudi;

4na Abishua, na Naamani, na Ahoa;

5na Gera, na Shufamu, na Huramu.

6Na hawa ndio wana wa Ehudi. (Hao ndio wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Geba; nao wakawachukua mateka mpaka Manahathi;

7na Naamani, na Ahoa, na Gera; aliwachukua mateka). Naye akamzaa Uza, na Ahihudi.

8Na Shaharaimu akazaa watoto katika Bara-Moabu, baada ya kuwafukuza wakeze Hushimu na Baara.

9Akazaliwa na Hodeshi, mkewe; Yobabu, na Sibia, na Mesha, na Malkamu;

10na Yeusi, na Shakia, na Mirma. Hao ndio wanawe, wakuu wa mbari za baba zao.

11Naye alikuwa amezaliwa na Hushimu, Abitubu, na Elpaali.

12Na wana wa Elpaali; Eberi, na Mishamu, na Shemedi, ambaye ndiye aliyejenga Ono na Lodi, pamoja na vijiji vyake;

13na Beria, na Shema, waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Aiyaloni, wale ambao waliwakimbiza wenyeji wa Gathi.

14Na Ahio, na Ghashaki, na Yeremothi;

15na Zebadia, na Aradi, na Ederi;

16na Mikaeli, na Ishpa, na Yoha; walikuwa wana wa Beria.

17Na Zebadia, na Meshulamu, na Hizki, na Heberi;

18na Ishmerai, na Izlia, na Yobabu; walikuwa wana wa Elpaali.

19Na Yakimu, na Zikri, na Zabdi;

20na Elienai, na Silethai, na Elieli;

21na Adaya, na Beraya, na Shimrathi; walikuwa wana wa Shema.

22Na Ishpani, na Eberi, na Elieli;

23na Abdoni, na Zikri, na Hanani;

24na Hanania, na Elamu, na Anthothiya;

25na Ifdeya, na Penueli; walikuwa wana wa Shashaki.

26Na Shamsherai, na Sheharia, na Athalia;

27na Yaareshia, na Eliya, na Zikri; walikuwa wana wa Yerohamu.

28Hao ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, katika vizazi vyao vyote, watu maarufu; na hao walikuwa wakikaa Yerusalemu.

29Basi huko Gibea alikaa babaye Gibea, jina lake Yeieli, ambaye jina la mkewe aliitwa Maaka;

30na mwanawe, mzaliwa wake wa kwanza, alikuwa Abdoni, na Suri, na Kishi, na Baali,

31na Gedori, na Ahio, na Zekaria

32Na Miklothi akamzaa Shimea. Na hao nao walikuwa wakikaa pamoja na ndugu zao huko Yerusalemu, kuwakabili ndugu zao.

33Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali.

34Na mwanawe Yonathani alikuwa Meribaali; na Meribaali akamzaa Mika.

35Na wana wa Mika; Pithoni, na Meleki, na Tarea, na Ahazi.

36Na Ahazi akamzaa Yara; na Yara akamzaa Alemethi, na Azmawethi, na Zimri; na Zimri akamzaa Mosa;

37na Mosa akamzaa Binea; na mwanawe huyo alikuwa Refaya, na mwanawe huyo ni Ekasa, na mwanawe huyo ni Aseli;

38naye Aseli alikuwa na wana sita, ambao majina yao ni haya; Azrikamu, na Bokeru, na Ishmaeli, na Shearia, na Obadia, na Hanani. Hao wote walikuwa wana wa Aseli.

39Na wana wa Esheki nduguye ni hawa; mzaliwa wake wa kwanza, Ulamu, na wa pili Yeushi, na wa tatu Elifeleti.

40Na wana wa Ulamu walikuwa watu hodari wa vita, wapiga upinde, nao walikuwa na wana wengi, na wana wa wana, watu mia na hamsini. Hao wote ndio waliokuwa wana wa Benyamini.