2 Samweli - Sura ya 22

2 Samweli - Sura ya 22

1Basi Daudi akamwambia Bwana maneno ya wimbo huu, siku ile Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake zote, na mkononi mwa Sauli;

2akasema, Bwana ndiye jabali langu, na ngome yangu, na mwokozi wangu, naam, wangu;

3Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye; Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, na makimbilio yangu; Mwokozi wangu, waniokoa na jeuri.

4Nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa; Hivyo nitaokoka na adui zangu.

5Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.

6Kamba za kuzimu zilinizunguka; Mitego ya mauti ikanikabili.

7Katika shida yangu nalimwita Bwana, Naam, nikamlalamikia Mungu wangu;

8Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka, Misingi ya mbinguni ikasuka-suka Na kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu.

9Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto ukatoka kinywani mwake ukala; Makaa yakawashwa nao.

10Aliziinamisha mbingu akashuka; Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake.

11Akapanda juu ya kerubi akaruka; Naam, alionekana juu ya mabawa ya upepo.

12Akafanya giza hema zake za kumzunguka, Makusanyiko ya maji, mawingu makuu ya mbinguni.

13Toka mwangaza uliokuwa mbele zake Makaa ya moto yakawashwa.

14Bwana alipiga radi toka mbinguni, Naye Aliye juu akaitoa sauti yake.

15Akapiga mishale, akawatawanya; Umeme, naye akawatapanya.

16Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Kwa kukemea kwake Bwana, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake.

17Alipeleka kutoka juu, akanishika; Akanitoa katika maji mengi;

18Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, Na wale walionichukia; Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi.

19Walinikabili siku ya msiba wangu; Lakini Bwana alikuwa tegemeo langu.

20Akanitoa akanipeleka panapo nafasi; Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.

21Bwana alinitendea sawasawa na haki yangu; Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa.

22Maana nimezishika njia za Bwana, Wala sikumwasi Mungu wangu.

23Maana hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu; Na kwa habari za amri zake, sikuziacha.

24Nami nalikuwa mkamilifu kwake, Nikajilinda na uovu wangu.

25Basi Bwana amenilipa sawasawa na haki yangu; Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.

26Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili Kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu;

27Kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu; Na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi.

28Na watu wanaoonewa wewe utawaokoa; Ila macho yako ni juu ya wenye kiburi, uwadhili.

29Kwa kuwa wewe u taa yangu, Ee Bwana; Na Bwana ataniangazia giza langu.

30Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi; Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta.

31Mungu njia yake ni kamilifu; Ahadi ya Bwana imehakikishwa; Yeye ndiye ngao yao Wote wanaomkimbilia.

32Maana ni nani aliye Mungu, ila Bwana? Ni nani aliye mwamba, ila Mungu wetu?

33Mungu ndiye ngome yangu yenye nguvu; Naye huwaongoza wakamilifu katika njia yake.

34Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu; Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.

35Ananifundisha mikono yangu vita; Hata mikono yangu yaupinda upinde wa shaba.

36Nawe umenipa ngao ya wokovu wako; Na unyenyekevu wako umenikuza.

37Umezifanyizia nafasi hatua zangu, Wala miguu yangu haikuteleza.

38Nimewafuatia adui zangu, na kuwaangamiza; Wala sikurudi nyuma hata walipokomeshwa.

39Nami nimewakomesha na kuwapiga-piga wasiweze kusimama; Naam, wameanguka chini ya miguu yangu.

40Maana umenifunga mshipi wa nguvu kwa vita; Umenitiishia chini yangu walioniondokea.

41Naam, adui zangu umewafanya wanipe visogo, Ili niwakatilie mbali wanaonichukia.

42Walitazama, lakini hakuna wa kuokoa; Walimwita Bwana, lakini hakuwajibu.

43Ndipo nikawaponda kama mavumbi ya nchi, Nikawakanyaga kama matope ya njiani, nikawatawanya.

44Nawe umeniokoa na mashindano ya watu wangu; Umenihifadhi niwe kichwa cha mataifa; Watu nisiowajua watanitumikia.

45Wageni watanijia wakinyenyekea; Kwa kusikia tu habari zangu, Mara watanitii.

46Wageni nao watatepetea, Watatoka katika ngome zao wakitetemeka.

47Bwana ndiye aliye hai; Na ahimidiwe mwamba wangu; Na atukuzwe Mungu wa mwamba wa wokovu wangu;

48Naam, Mungu anipatiaye kisasi, Na kuwatweza watu chini yangu,

49Na kunileta nje nitoke kwa adui zangu; Naam, waniinua juu yao walioniinukia; Waniponya na mtu wa jeuri.

50Basi, Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako.

51Ampa mfalme wake wokovu mkuu; Amfanyia fadhili masihi