Mwanzo - Sura ya 36

1Hivi ndivyo vizazi vya Esau, ndiye Edomu.
2Esau alitwaa binti za Kanaani, kuwa wakeze; Ada, binti Eloni, Mhiti, na Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, Mhivi;
3na Basemathi, binti Ishmaeli, nduguye Nebayothi.
4Ada akamzalia Esau Elifazi; na Basemathi alizaa Reueli.
5Oholibama alizaa Yeushi, na Yalamu, na Kora. Hao ndio wana wa Esau aliozaliwa katika nchi ya Kanaani.
6Esau akawatwaa wakeze, na wanawe, na binti zake, na watu wote wa nyumbani mwake, na ng'ombe zake, na wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyoyapata katika nchi ya Kanaani; akaenda mpaka nchi iliyo mbali na Yakobo nduguye.
7Maana mali yao yalikuwa mengi wasiweze kukaa pamoja, wala haikuweza nchi ya kusafiri kwao kuwachukua, kwa sababu ya wanyama wao.
8Esau akakaa katika mlima Seiri, Esau ndiye Edomu.
9Hivi ni vizazi vya Esau, baba ya Edomu katika mlima Seiri.
10Haya ndiyo majina ya wana wa Esau; Elifazi, mwana wa Ada mkewe Esau. Reuli, mwana wa Basemathi, mkewe Esau.
11Na wana wa Elifazi, ni Temani na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi.
12Na Timna alikuwa suria wa Elifazi, mwana wa Esau; naye akamzalia Elifazi Amaleki. Hao ndio wana wa Ada, mkewe Esau.
13Na hawa ni wana wa Reueli, Nahathi, na Zera, na Shama na Miza. Hao walikuwa wana wa Basemathi, mkewe Esau.
14Na hawa ni wana wa Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, mkewe Esau; akamzalia Esau, Yeushi, na Yalamu, na Kora.
15Hawa ndio majumbe wao wana wa Esau; wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau; jumbe Temani, jumbe Omari, jumbe Sefo, jumbe Kenazi,
16jumbe Kora, jumbe Gatamu, jumbe Amaleki. Hao ndio majumbe, waliotoka kwa Elifazi katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Ada.
17Na hawa ni wana wa Reueli, mwanawe Esau; jumbe Nahathi, jumbe Zera, jumbe Shama, jumbe Miza. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Reueli katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Basemathi, mkewe Esau.
18Na hawa ni wana wa Oholibama, mkewe Esau; jumbe Yeushi, jumbe Yalamu, jumbe Kora. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Oholibama, binti Ana, mkewe Esau.
19Hao ni wana wa Esau, na hao ndio majumbe wao; naye Esau ndiye Edomu.
20Hawa ni wana wa Seiri, Mhori, wenyeji wa nchi ile; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana,
21na Dishoni, na Eseri, na Dishani. Hao ndio majumbe waliotoka katika Wahori, wana wa Seiri, katika nchi ya Edomu.
22Na wana wa Lotani, ni Hori, na Hemamu; na umbu lake Lotani ni Timna.
23Na hawa ni wana wa Shobali, Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu.
24Na hawa ni wana wa Sibeoni, Aya, na Ana; ni yule Ana aliyeona chemchemi za maji ya moto katika jangwa, alipokuwa akichunga punda za Sibeoni babaye.
25Na hawa ni wana wa Ana, Dishoni, na Oholibama, binti Ana.
26Na hawa ni wana wa Dishoni, Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani.
27Na hawa ni wana wa Eseri, Bilhani, na Zaawani, na Akani.
28Na hawa ni wana wa Dishani, Usi, na Arani.
29Hawa ndio majumbe waliotoka katika Wahori; jumbe Lotani, jumbe Shobali, jumbe Sibeoni, jumbe Ana,
30jumbe Dishoni, jumbe Eseri jumbe Dishani. Hao ndio majumbe waliotoka katika Wahori, kwa habari za majumbe yao, katika nchi ya Seiri.
31Na hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla ya kumiliki mfalme ye yote juu ya wana wa Israeli.
32Bela wa Beori alimiliki katika Edomu, na jina la mji wake ni Dinhaba.
33Akafa Bela, akamiliki Yobabu mwana wa Zera, wa Bosra, badala yake.
34Akafa Yobabu, akamiliki Hushamu, wa nchi ya Watemani, badala yake.
35Akafa Hushamu, akamiliki Hadadi wa Bedadi badala yake, naye ndiye aliyepiga Midiani katika nyika ya Moabu, na jina la mji wake ni Avithi.
36Akafa Hadadi, akamiliki Samla wa Masreka badala yake.
37Akafa Samla, na Shauli wa Rehobothi, ulio karibu na mto, akamiliki badala yake.
38Akafa Shauli, akamiliki Baal-hanani, mwana wa Akbori, badala yake.
39Akafa Baal-hanani, mwana wa Akbori, akamiliki Hadadi badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu.
40Na hayo ndiyo majina ya majumbe waliotoka kwa Esau, kufuata jamaa zao, na mahali pao, kwa majina yao. Jumbe Timna, jumbe Alva, jumbe Yethethi,
41jumbe Oholibama, jumbe Ela, jumbe Pinoni,
42jumbe Kenazi, jumbe Temani, jumbe Mibsari,
43jumbe Magdieli, jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu, kufuata makao yao, katika nchi ya mamlaka yao. Naye huyo ndiye Esau, baba ya Edomu.