Mwanzo - Sura ya 9

Mwanzo - Sura ya 9

1Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi.

2Kila mnyama wa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani: pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu.

3Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote.

4Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.

5Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu.

6Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.

7Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi, mkaongezeke ndani yake.

8Mungu akamwambia Nuhu, na wanawe pamoja naye, akisema,

9Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu;

10tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi.

11Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi.

12Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele;

13Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.

14Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni,

15nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili.

16Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi.

17Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi.

18Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani.

19Hawa watatu walikuwa wana wa Nuhu na kwa hao nchi yote ikaenea watu.

20Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;

21akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.

22Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.

23Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.

24Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.

25Akasema,

26Akasema,

27Mungu akamnafisishe Yafethi.

28Na Nuhu akaishi baada ya ile gharika miaka mia tatu na hamsini.

29Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafa.