Waebrania - Sura ya 1

1Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,
2mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
3Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;
4amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao.
5Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa?
6Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema,
7Na kwa habari za malaika asema,
8Lakini kwa habari za Mwana asema,
9Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio.
10Na tena,
11Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu; Nazo zote zitachakaa kama nguo,
12Na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika; Lakini wewe u yeye yule, Na miaka yako haitakoma.
13Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote,
14Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?