Yoshua - Sura ya 12

1Basi hawa ndio wafalme wa nchi, ambao wana wa Israeli waliwapiga na kuimiliki nchi yao ng'ambo ya pili ya Yordani, upande wa maawio ya jua, kutoka bonde la Amoni mpaka mlima wa Hermoni, na nchi yote ya Araba upande wa mashariki;
2Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekaa huko Heshboni, naye ndiye aliyetawala toka Aroeri, ulioko kando ya bonde la Arnoni, na toka huo mji ulio katikati ya bonde, na nusu ya Gileadi, hata kuufikilia mto wa Yaboki, mpaka wa hao wana wa Amoni;
3na nchi ya Araba mpaka bahari ya Kinerethi, kuelekea mashariki, tena mpaka bahari ya Ataba, mpaka Bahari ya Chumvi, kwendea mashariki, njia ya kwendea Beth-yeshimothi; tena upande wa kusini, chini ya matelemko ya Pisga;
4tena mpaka wa Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa wa hayo mabaki ya hao Warefai, aliyekaa Ashtarothi na Edrei,
5naye alitawala katika mlima wa Hermoni, na katika Saleka, na katika Bashani yote, hata mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka, na nusu ya Gileadi, mpaka wa huyo Sihoni mfalme wa Heshboni.
6Musa mtumishi wa Bwana na wana wa Israeli wakawapiga; naye Musa mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila ya Manase iwe urithi wao.
7Hawa ni wafalme wa hiyo nchi ambao Yoshua na wana wa Israeli waliwapiga ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa magharibi, kutoka Baal-gadi katika bonde la Lebanoni mpaka kilima cha Halaki, kilichoelekea Seiri; Yoshua naye akawapa kabila za Israeli iwe milki yao sawasawa na magawanyo yao;
8katika nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika nchi ya Araba, na katika matelemko, na katika bara, na katika Negebu; nchi ya Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi;
9mfalme wa Yeriko, mmoja; mfalme wa Ai, ulio karibu na Betheli, mmoja;
10mfalme wa Yerusalemu, mmoja; mfalme wa Hebroni, mmoja;
11mfalme wa Yarmuthi, mmoja; na mfalme wa Lakishi, mmoja;
12mfalme wa Egloni, mmoja; na mfalme wa Gezeri, mmoja;
13mfalme wa Debiri, mmoja; na mfalme wa Gederi, mmoja;
14mfalme wa Horma, mmoja; na mfalme wa Aradi, mmoja;
15mfalme wa Libna, mmoja; na mfalme wa Adulamu, mmoja;
16mfalme wa Makeda, mmoja; na mfalme wa Betheli, mmoja;
17mfalme wa Tapua, mmoja; na mfalme wa Heferi, mmoja;
18mfalme wa Afeka, mmoja; na mfalme wa Lasharoni, mmoja;
19mfalme wa Madoni, mmoja; na mfalme wa Hazori, mmoja;
20mfalme wa Shimron-meroni, mmoja; na mfalme wa Akshafu, mmoja;
21mfalme wa Taanaki, mmoja; na mfalme wa Megido, mmoja;
22na mfalme wa Kedeshi, mmoja; mfalme wa Yokneamu wa Karmeli, mmoja;
23mfalme wa Dori katika kilima cha Dori, mmoja; na mfalme wa makabila katika Gilgali, mmoja;
24na mfalme wa Tirsa, mmoja; wafalme hao wote walikuwa ni thelathini na mmoja.