Yoshua - Sura ya 19

Yoshua - Sura ya 19

1Kisha kura ya pili ilitokea kwa ajili ya Simeoni, maana, kwa ajili ya hiyo kabila ya wana wa Simeoni, kwa kuandama jamaa zao; na urithi wao ulikuwa katikati ya urithi wa wana wa Yuda.

2Miji waliyokuwa nayo katika urithi wao ni Beer-sheba, na Sheba, na Molada;

3na Hasarshuali, na Bala, na Esemu;

4na Eltoladi, na Bethuli, na Horma;

5na Siklagi, na Bethmarkabothi, na Hasarsusa;

6na Bethlebaothi, na Sharuheni; miji kumi na mitatu, pamoja na vijiji vyake;

7na Aini, na Rimoni, na Etheri, na Ashani; miji minne, pamoja na vijiji vyake;

8tena vijiji vyote vilivyozunguka miji hiyo kote kote mpaka Baalath-beeri, Rama wa Kusini. Huo ndio urithi wa kabila ya wana wa Simeoni kwa kuandama jamaa zao.

9Huo urithi wa hao wana wa Simeoni ulitoka katika fungu la wana wa Yuda; kwa maana hilo fungu la wana wa Yuda lilikuwa ni kubwa mno kwao; kwa hiyo wana wa Simeoni walikuwa na urithi katikati ya urithi wao.

10Kisha kura ya tatu ilitokea kwa ajili ya wana wa Zabuloni kwa kuandama jamaa zao; na mpaka wa urithi wao ulifikilia hata Saridi;

11kisha mpaka wao ukakwea kwendelea upande wa magharibi, hata kufikilia Marala, nao ukafikilia hata Dabeshethi; nao ukafikilia kijito cha maji kilicho mkabala wa Yokneamu;

12kisha ukazunguka kutoka Saridi kwendelea upande wa mashariki kwa kuelekea maawio ya jua hata kufikilia mpaka wa Kisiloth-ubori; kisha ukatokea hata Daberathi, kisha ukakwea kwendelea Yafia;

13kutoka hapo ukaendelea kuelekea mashariki mpaka Gath-heferi, hata kufikilia Ethkasini; kisha ukatokea huko Rimoni ufikiliao hata Nea;

14kisha mpaka uliizunguka nchi hiyo kwa upande wa kaskazini hata Hanathoni; kisha matokeo yake yalikuwa katika bonde la Iftaeli;

15na Katathi, na Nahalali, na Shimroni, na Idala, na Bethlehemu; miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.

16Huu ndio urithi wa wana wa Zabuloni kwa kuandama jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.

17Kisha kura ya nne ilitokea kwa ajili ya Isakari, maana, ni kwa ajili ya wana wa Isakari kwa kuandama jamaa zao.

18Na mpaka wao ulifikilia Yezreeli, na Kesulothi, na Shunemu;

19na Hafaraimu, na Shioni, na Anaharathi;

20na Rabithu, na Kishioni, na Ebesi;

21na Remethi, na Enganimu, na Enhada, na Bethpasesi;

22na mpaka ukafikilia hata Tabori, na Shahasuma na Bethshemeshi; na matokeo ya mpaka wao yalikuwa katika mto wa Yordani; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.

23Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Isakari kwa kuandama jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.

24Kisha kura ya tano ilitokea kwa ajili ya kabila ya wana wa Asheri kwa kuandama jamaa zao.

25Na mpaka wao ulikuwa ni Helkathi, na Hali, na Beteni, na Akishafu;

26na Alameleki, na Amadi, na Mishali; nao ukafikilia hata Karmeli upande wa magharibi, tena ulifikilia hata Shihor-libnathi;

27kisha ukazunguka kuelekea maawio ya jua mpaka Beth-dagoni, nao ukafikilia hata Zabuloni, tena mpaka bonde la Iftaeli upande wa kaskazini hata Bethemeki na Neyeli; kisha ukatokea hata Kabuli upande wa kushoto;

28na Ebroni, na Rehobu, na Hamoni, na Kana, hata kufikilia Sidoni mkuu;

29kisha mpaka ulizunguka kuelekea Rama, na mji wa Tiro ulio na boma; kisha mpaka ulizunguka kuelekea Hosa; na matokeo yake yalikuwa baharini katika nchi ya Akzibu;

30na Uma pia, na Afeka, na Rehobu; miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.

31Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Asheri kwa kuandama jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.

32Kisha kura ya sita ikatokea kwa ajili ya wana wa Naftali, maana, ni kwa ajili ya wana wa Naftali kwa kuandama jamaa zao.

33Na mpaka wao ulikuwa kutoka Helefu, tokea ule mwaloni ulio katika Saananimu, na Adami-nekebu, na Yabineeli, hata kufikilia Lakumu; na matokeo yake yalikuwa katika mto wa Yordani;

34tena mpaka ulizunguka kwendelea upande wa magharibi hata Aznoth-tabori, tena kutoka hapo ukaendelea mpaka Hukoki; kisha ukafikilia hata Zabuloni upande wa kusini, tena ulifikilia hata Asheri upande wa magharibi, tena ulifikilia hata Yuda hapo katika mto wa Yordani kwa upande wa kuelekea maawio ya jua.

35Na miji yenye boma ilikuwa ni hii, Sidimu, na Seri, na Hamathi, na Rakathi, na Kinerethi;

36na Adama, na Rama, na Hazori;

37na Kedeshi, na Edrei, na Enhasori;

38na Ironi, na Migdal-eli, na Horemu, na Bethanathi, na Bethshemeshi; miji kumi na kenda, pamoja na vijiji vyake.

39Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Naftali kwa kuandama jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.

40Kisha kura ya saba ilitokea kwa ajili ya kabila ya wana wa Dani kwa kuandama jamaa zao.

41Na mpaka wa urithi wao ulikuwa ni Sora, na Eshtaoli, na Irishemeshi;

42na Shaalabini, na Aiyaloni, na Ithla;

43na Eloni, na Timna, na Ekroni;

44na Elteka, na Gibethoni, na Baalathi;

45na Yehudi, na Bene-beraki, na Gathrimoni;

46na Meyarkoni, na Rakoni, pamoja na huo mpaka uliokuwa mkabala wa Yafa.

47Kisha mpaka wa wana wa Dani ulitokea kuwapita wao; kwa kuwa hao wana wa Dani wakakwea na kupigana na Leshemu, na kuutwaa, na kuupiga kwa makali ya upanga, na kuumiliki, nao wakakaa humo, wakauita Dani, kwa kuliandama jina la huyo Dani mzee wao.

48Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Dani kwa kuandama jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.

49Basi wakamaliza hiyo kazi yao ya kuigawanya nchi iwe urithi kwa kuandama mipaka yake; kisha wana wa Israeli wakampa Yoshua, mwana wa Nuni, urithi katikati yao;

50sawasawa na ile amri ya Bwana wakampa mji alioutaka, maana, ni Timnath-sera katika nchi ya vilima ya Efraimu; naye akaujenga huo mji na kukaa mumo.

51Hizi ndizo nchi, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua huyo mwana wa Nuni, pamoja na hao vichwa vya nyumba za mababa ya kabila za wana wa Israeli, walizigawanya kwa njia ya kupiga kura, ziwe urithi, huko Shilo mbele ya Bwana, hapo mlangoni mwa hema ya kukutania. Basi hivyo wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.