Nehemia - Sura ya 10

Nehemia - Sura ya 10

1Basi hawa ndio waliotia muhuri; Nehemia, ndiye Tirshatha, mwana wa Hakalia, na Sedekia;

2Seraya, Azaria, Yeremia;

3Pashuri, Amaria, Malkiya;

4Hamshi, Shekania, Maluki;

5Harimu, Meremothi, Obadia;

6Danieli, Ginethoni, Baruki;

7Meshulamu, Abiya, Miyamini;

8Maazia, Bilgai, Shemaya; hao ndio waliokuwa makuhani.

9Na Walawi; ndio, Yeshua, mwana wa Azania, Binui wa wana wa Henadadi, Kadmieli;

10na ndugu zao, Shebania, Hodia, Kelita, Pelaya, Hanani;

11Mika, Rehobu, Hashabia;

12Zakuri, Sherebia, Shebania;

13Hodia, Bani, Beninu;

14Na wakuu wa watu; Paroshi, Pahath-Moabu, Elamu, Zatu, Bani;

15Buni, Azgadi, Bebai;

16Adonikamu, Bigwai, Adini;

17Ateri, Hezakia, Azuri;

18Hodia, Hashumu, Besai;

19Harifu, Anathothi, Nobai;

20Magpiashi, Meshulamu, Heziri;

21Meshezabeli, Sadoki, Yadua;

22Pelatia, Hanani, Anaya;

23Hoshea, Hanania, Hashubu;

24Haloheshi, Pilha, Shobeki;

25Rehumu, Hashabna, Maaseya;

26Ahia, Hanani, Anani;

27Maluki, Harimu, na Baana.

28Na watu waliosalia, makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, Wanethini, na hao wote waliojitenga katika watu wa nchi kwa torati ya Mungu; wake zao, na wana wao, na binti zao, kila mwenye maarifa na akili;

29wakaambatana na ndugu zao, wakuu wao, nao wakaingia katika laana na kiapo, ya kuwa wataiendea torati ya Mungu, iliyotolewa kwa mkono wa Musa, mtumishi wa Mungu, na kuziangalia, na kuzitenda, amri zote za Bwana, Bwana wetu, na hukumu zake na sheria zake;

30wala tusiwaoze watu wa nchi binti zetu, wala kuwatwalia wana wetu binti zao;

31tena watu wa nchi wakitembeza biashara, au chakula cho chote, siku ya sabato, tusinunue kwao siku ya sabato, au siku takatifu; tena kwamba tuuache mwaka wa saba, na madai ya kila deni.

32Tena tukajifanyia maagizo, kujitoza mwaka kwa mwaka theluthi ya shekeli kwa huduma ya nyumba ya Mungu wetu;

33kwa mikate ya wonyesho, na kwa sadaka ya unga ya daima, na kwa sadaka ya kuteketezwa ya daima, ya sabato, na ya siku za mwezi mpya, na ya sikukuu, tena kwa vitu vile vitakatifu, na kwa sadaka za dhambi, za kuwafanyia Israeli upatanisho, na kwa ajili ya kazi yote ya nyumba ya Mungu wetu.

34Kisha tukapiga kura, makuhani, na Walawi, na watu, juu ya matoleo ya kuni, ili kuzileta nyumbani kwa Mungu wetu, kwa kadiri ya mbari za baba zetu, kwa nyakati zilizoamriwa, mwaka kwa mwaka, kukoka moto madhabahuni mwa Bwana, Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika torati;

35tena kuleta malimbuko ya ardhi yetu, na malimbuko ya matunda yote ya miti ya namna zote, mwaka kwa mwaka, nyumbani kwa Bwana;

36tena wazaliwa wa kwanza wa wana wetu, na wa wanyama wetu, kama ilivyoandikwa katika torati, na wazaliwa wa kwanza wa ng'ombe zetu na kondoo zetu, ili kuwaleta nyumbani mwa Mungu wetu, kwa makuhani watumikao nyumbani mwa Mungu wetu;

37tena tuyalete malimbuko ya unga wetu, na sadaka zetu za kuinuliwa, na matunda ya miti ya namna zote, mvinyo, na mafuta, kwa makuhani, hapo vyumbani kwa nyumba ya Mungu wetu; na zaka za ardhi yetu kwa Walawi; kwa kuwa hao Walawi wazitwaa zaka mijini mwote mwa kulima kwetu.

38Naye kuhani, mwana wa Haruni, atakuwako pamoja na Walawi, watwaapo zaka Walawi; nao Walawi wataipandisha zaka ya hizo zaka nyumbani kwa Mungu wetu, vyumbani, katika nyumba ya hazina.

39Kwa kuwa wana wa Israeli na wana wa Lawi wataleta sadaka ya kuinuliwa ya nafaka, na mvinyo, na mafuta, vyumbani, kwa kuwa ndimo vilimo vyombo vya patakatifu, na makuhani watumikao, na mabawabu, na waimbaji; wala sisi hatutaiacha nyumba ya Mungu wetu.