Nehemia - Sura ya 7

1Ikawa, hapo ukuta ulipojengwa, na milango nimekwisha kuisimamisha, na mabawabu, na waimbaji, na Walawi, wamewekwa,
2ndipo nilimwagiza ndugu yangu, Hanani, pamoja na yule Hanania, jemadari wa ngome, kuwa na amri juu ya Yerusalemu; kwa maana alikuwa mtu mwaminifu huyo, na mwenye kumcha Mungu kuliko wengi.
3Nikawaambia, Yasifunguliwe malango ya Yerusalemu kabla halijachomoza jua; nao walinzi wangali wakisimama bado, waifunge milango, mkaikaze; kisha wekeni walinzi wa zamu wa hao wakaao Yerusalemu, kila mtu na zamu yake, na kila mtu kuielekea nyumba yake.
4Basi mji ulikuwa wa nafasi nyingi, tena mkubwa; lakini watu waliomo walikuwa haba, wala nyumba hazijajengwa.
5Mungu wangu akanitia moyoni mwangu, kwamba niwakusanye wakuu na mashehe, na watu, ili wahesabiwe kwa nasaba. Nikakiona kitabu cha vizazi vya hao waliokwea hapo kwanza, nikaona ya kwamba imeandikwa humo;
6Hawa ndio wana wa wilaya, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadreza,
7ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo hesabu ya wanaume wa watu wa Israeli;
8Wana wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili.
9Wana wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili.
10Wana wa Ara mia sita hamsini na wawili.
11Wana wa Pahath-Moabu, wa wana wa Yeshua na Yoabu, elfu mbili mia nane na kumi na wanane.
12Wana wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.
13Wana wa Zatu, mia nane arobaini na watano.
14Wana wa Zakai, mia saba na sitini.
15Wana wa Binui, mia sita arobaini na wanane.
16Wana wa Bebai, mia sita ishirini na wanane.
17Wana wa Azgadi, elfu mbili mia tatu ishirini na wawili.
18Wana wa Adonikamu, mia sita sitini na saba.
19Wana wa Bigwai, elfu mbili sitini na saba.
20Wana wa Adini, mia sita hamsini na watano.
21Wana wa Ateri, wa Hezekia, tisini na wanane.
22Wana wa Hashumu, mia tatu ishirini na wanane.
23Wana wa Besai, mia tatu ishirini na wanne.
24Wana wa Harifu, mia moja na kumi na wawili.
25Wana wa Gibeoni, tisini na watano.
26Watu wa Bethlehemu na Netofa, mia na themanini na wanane.
27Watu wa Anathothi, mia na ishirini na wanane.
28Watu wa Beth-Azmawethi, arobaini na wawili.
29Watu wa Kiriath-Yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arobaini na watatu.
30Watu wa Rama na Geba, mia sita na ishirini na mmoja.
31Watu wa Mikmashi, mia moja na ishirini na wawili.
32Watu wa Betheli na Ai, mia moja ishirini na watatu.
33Watu wa Nebo, hamsini na wawili.
34Wana wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.
35Wana wa Harimu, mia tatu na ishirini.
36Wana wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano.
37Wana wa Lodi, na Hadidi, na Ono, mia saba ishirini na mmoja.
38Watu wa Senaa, elfu tatu mia kenda na thelathini.
39Makuhani; Wana wa Yedaya, wa mbari ya Yeshua, mia kenda sabini na watatu.
40Wana wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili.
41Wana wa Pashuri, elfu moja mia mbili arobaini na saba.
42Wana wa Harimu, elfu moja na kumi na saba.
43Walawi; Wana wa Yeshua, wa Kadmieli wa wana wa Hodavia, sabini na wanne.
44Waimbaji; Wana wa Asafu, mia moja arobaini na wanane.
45Mabawabu; Wana wa Shalumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni, wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Shobai, mia moja thelathini na wanane.
46Wanethini; wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaothi;
47wana wa Kerosi, wana wa Siaha, wana wa Padoni;
48wana wa Lebana, wana wa Hagaba, wana wa Salmai;
49wana wa Hanani, wana wa Gideli, wana wa Gahari;
50wana wa Reaya, wana wa Resini, wana wa Nekoda;
51wana wa Gazamu, wana wa Uza, wana wa Pasea;
52wana wa Besai wana wa Meunimu, wana wa Nefusimu;
53wana wa Bakbuki, wana wa Hakufa, wana wa Harhuri;
54wana wa Basluthi, wana wa Mehida, wana wa Harsha;
55wana wa Barkosi, wana wa Sisera, wana wa Tema;
56wana wa Nesia, wana wa Hatifa.
57Akina watumwa wa Sulemani; Wana wa Sotai, wana wa Soferethi, wana wa Peruda;
58wana wa Yaala, wana wa Darkoni, wana wa Gideli;
59wana wa Shefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokereth-Sebaimu, wana wa Amoni.
60Wanethini wote, pamoja na akina watumwa wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili.
61Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; walakini hawakuweza kuonyesha mbari za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli;
62Wana wa Delaya, wana wa Tobia, wana wa Nekoda, mia sita na arobaini na wawili.
63Tena katika makuhani; Wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo binti Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao.
64Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi.
65Na huyo Tirshatha
66Basi hilo kusanyiko lote zima, jumla yake ilikuwa watu arobaini na mbili elfu na mia tatu na sitini,
67tena zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao waume kwa wake, ambao walikuwa elfu saba na mia tatu na thelathini na saba; kisha walikuwa na waimbaji waume kwa wake mia mbili arobaini na watano.
68Farasi zao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu zao, mia mbili arobaini na watano;
69ngamia zao, mia nne thelathini na watano; punda zao, elfu sita na mia saba na ishirini.
70Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa walitoa mali kwa ajili ya kazi hii. Yule Tirshatha akatoa kwa ajili ya hazina darkoni
71Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa wakatoa, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu ishirini elfu, na mane
72Na mabaki ya watu wakatoa darkoni za dhahabu ishirini elfu, na mane za fedha elfu mbili, na mavazi ya makuhani sitini na saba.
73Hivyo makuhani, na Walawi, na mabawabu, na waimbaji, na baadhi ya watu, na Wanethini, na Israeli wote, wakakaa mijini mwao. Hata ulipowadia mwezi wa saba, wana wa Islaeli walikuwa wakikaa katika miji yao.