Hesabu - Sura ya 33

1Hizi ndizo safari za wana wa Israeli, hapo walipotoka nchi ya Misri kwa jeshi zao chini ya mkono wa Musa na Haruni.
2Musa akaandika jinsi walivyotoka katika safari zao, kwa amri ya Bwana; na hizi ndizo safari zao kama kutoka kwao kulivyokuwa.
3Wakasafiri kutoka Ramesesi mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza; siku ya pili baada ya Pasaka, wana wa Israeli wakatoka kwa mkono wa nguvu mbele ya macho ya Wamisri wote,
4hapo Wamisri walipokuwa wanazika wazaliwa wa kwanza wao wote, Bwana aliokuwa amewapiga kati yao; Bwana akafanya hukumu juu ya miungu yao nayo.
5Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi, wakapanga katika Sukothi.
6Kisha wakasafiri kutoka Sukothi, wakapanga Ethamu, palipo katika mwisho wa nyika.
7Wakasafiri kutoka Ethamu, na kurudi nyuma hata Pi-hahirothi palipokabili Baal-sefoni; wakapanga mbele ya Migdoli.
8Wakasafiri kutoka hapo mbele ya Hahirothi, wakapita katikati ya bahari na kuingia jangwani; kisha wakaenda safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu, wakapanga Mara.
9Wakasafiri kutoka Mara, wakafikilia Elimu; huko Elimu palikuwa na chemchemi za maji kumi na mbili, na mitende sabini; nao wakapanga hapo.
10Wakasafiri kutoka Elimu wakapanga karibu na Bahari ya Shamu.
11Wakasafiri kutoka Bahari ya Shamu, wakapanga katika nyika ya Sini.
12Wakasafiri kutoka nyika ya Sini, wakapanga Dofka.
13Wakasafiri kutoka Dofka, wakapanga Alushi.
14Wakasafiri kutoka Alushi, wakapanga Refidimu, ambapo hapakuwa na maji ya watu kunywa.
15Wakasafiri kutoka Refidimu, wakapanga katika nyika ya Sinai.
16Wakasafiri kutoka nyika ya Sinai, wakapanga Kibroth-hataava.
17Wakasafiri kutoka Kibroth-hataava, wakapanga Haserothi.
18Wakasafiri kutoka Haserothi, wakapanga Rithma.
19Wakasafiri kutoka Rithma, wakapanga Rimon-peresi.
20Wakasafiri kutoka Rimon-peresi, wakapanga Libna.
21Wakasafiri kutoka Libna, wakapanga Risa.
22Wakasafiri kutoka Risa, wakapanga Keheletha.
23Wakasafiri kutoka Keheletha, wakapanga katika mlima wa Sheferi
24Wakasafiri kutoka huo mlima wa Sheferi, wakapanga Harada.
25Wakasafiri kutoka Harada, wakapanga Makelothi.
26Wakasafiri kutoka Makelothi, wakapanga Tahathi.
27Wakasafiri kutoka Tahathi wakapanga Tera.
28Wakasafiri kutoka Tera, wakapanga Mithka.
29Wakasafiri kutoka Mithka, wakapanga Hashmona.
30Wakasafiri kutoka Hashmona, wakapanga Moserothi.
31Wakasafiri kutoka Moserothi, wakapanga Bene-yakani.
32Wakasafiri kutoka Bene-yakani, wakapanga Hor-hagidgadi.
33Wakasafiri kutoka Hor-hagidgadi, wakapanga Yotbatha.
34Wakasafiri kutoka Yotbatha, wakapanga Abrona.
35Wakasafiri kutoka Abrona, wakapanga Esion-geberi.
36Wakasafiri kutoka Esion-geberi, wakapanga katika nyika ya Sini (ni Kadeshi).
37Wakasafiri kutoka Kadeshi wakapanga katika mlima wa Hori, katika mpaka wa nchi ya Edomu,
38Haruni akakwea mlima wa Hori, kwa amri ya Bwana, akafa hapo, katika mwaka wa arobaini baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, mwezi wa tano, siku ya kwanza ya mwezi.
39Naye Haruni alikuwa mtu wa umri wa miaka mia na ishirini na mitatu hapo alipokufa katika mlima wa Hori.
40Ndipo Mkanaani, mfalme wa Aradi, aliyekaa pande za Negebu katika nchi ya Kanaani akasikia habari za kuja kwao wana wa Israeli.
41Nao wakasafiri kutoka mlima wa Hori, wakapanga Salmona.
42Wakasafiri kutoka Salmona, wakapanga Punoni.
43Wakasafiri kutoka Punoni, wakapanga Obothi.
44Wakasafiri kutoka Obothi, wakapanga Iye-abarimu, katika mpaka wa Moabu.
45Wakasafiri kutoka Iye-abarimu, wakapanga Dibon-gadi.
46Wakasafiri kutoka Dibon-gadi, wakapanga Almon-diblathaimu.
47Wakasafiri kutoka Almon-diblathaimu, wakapanga katika milima ya Abarimu, kukabili Nebo.
48Wakasafiri kutoka hiyo milima ya Abarimu, wakapanga katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo Yeriko.
49Wakapanga karibu na Yordani, tangu Beth-yeshimothi hata kufikilia Abel-shitimu katika nchi tambarare za Moabu.
50Kisha Bwana akanena na Musa hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko, na kumwambia,
51Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapovuka mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani,
52ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote wa hiyo nchi mbele yenu, nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu, na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunja-vunja mahali pao pote palipoinuka;
53nanyi mtaishika hiyo nchi kuimiliki na kuketi humo; kwa kuwa mimi nimewapa ninyi hiyo nchi ili mwimiliki.
54Nanyi mtairithi nchi kwa kufanya kura, kama jamaa zenu zilivyo; hao walio wengi mtawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka utawapa kama kupunguka kwao; mahali po pote kura itakapomwangukia mtu ye yote, mahali hapo ni pake; mtarithi kama kabila za baba zenu zilivyo.
55Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu; ndipo hao ambao mtakaowasaza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mwakaa.
56Kisha itakuwa, kama nilivyoazimia kuwatenda wao, ndivyo nitakavyowatenda ninyi.