Hesabu - Sura ya 7

Hesabu - Sura ya 7

1Ilikuwa siku hiyo Musa alipokwisha kuisimamisha maskani, na kuitia mafuta, na kuitakasa, na vyombo vyake vyote, na hiyo madhabahu na vyombo vyake vyote, na kuvitia mafuta, na kuvitakasa;

2ndipo wakuu wa Israeli, vichwa vya nyumba za baba zao, wakatoa matoleo; hao ndio wakuu wa kabila, hao ndio waliokuwa juu yao waliohesabiwa;

3nao wakamletea Bwana matoleo yao, magari sita yenye mafuniko juu, na ng'ombe kumi na wawili; gari moja kwa wakuu wawili wawili, na ng'ombe mmoja kwa kila mkuu; nao wakayasongeza hapo mbele ya maskani.

4Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

5Pokea mikononi mwao, ili kwamba viwe vya kutumiwa katika utumishi wa hema ya kukutania; nawe utawapa Walawi vitu hivyo, kila mtu utampa kama utumishi wake ulivyo.

6Basi Musa akapokea hayo magari, na ng'ombe, akawapa Walawi.

7Wana wa Gershoni akawapa magari mawili na ng'ombe wanne, kama utumishi wao ulivyokuwa;

8na wana wa Merari akawapa magari manne na ng'ombe wanane kama utumishi wao ulivyokuwa, chini ya mkono wa Ithamari, mwana wa Haruni kuhani.

9Lakini hakuwapa wana wa Kohathi; maana, utumishi wa vile vitu vitakatifu ulikuwa ni wao; nao wakavichukua mabegani mwao.

10Kisha wale wakuu wakatoa matoleo kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, katika siku hiyo iliyotiwa mafuta, wakuu wakayatoa matoleo yao mbele ya madhabahu.

11Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Watasongeza matoleo yao, kila mkuu kwa siku yake, kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu.

12Basi aliyetoa matoleo yake siku ya kwanza ni Nashoni mwana wa Aminadabu, wa kabila ya Yuda;

13na matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha uzani wake ni shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga;

14na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kimejaa uvumba;

15ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mmoja mume, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

16mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

17na kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe waume wawili, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Nashoni mwana wa Aminadabu.

18Siku ya pili Nethaneli mwana wa Suari, mkuu wa Isakari, alitoa;

19yeye akasongeza matoleo yake, sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa ni sadaka ya unga;

20na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilikuwa kimejaa uvumba;

21na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

22na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

23na kwa dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Nethaneli mwana wa Suari.

24Siku ya tatu Eliabu mwana wa Heloni, mkuu wa wana wa Zabuloni;

25matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;

26na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;

27na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

28na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

29tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Eliabu mwana wa Heloni.

30Siku ya nne Elisuri mwana wa Shedeuri, mkuu wa wana wa Reubeni;

31matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;

32na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;

33na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

34na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

35tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Elisuri mwana wa Shedeuri.

36Siku ya tano Shelumieli mwana wa Suri-shadai, mkuu wa wana Simeoni;

37matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;

38na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;

39na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

40na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

41tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Shelumieli mwana wa Suri-shadai

42Siku ya sita Eliasafu mwana wa Deueli, mkuu wa wana wa Gadi

43matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;

44na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;

45na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

46na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

47tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Eliasafu mwana wa Deueli.

48Siku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, mkuu wa wana wa Efraimu;

49matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;

50na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;

51na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

52na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

53tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Elishama mwana wa Amihudi.

54Siku ya nane Gamalieli mwana wa Pedasuri, mkuu wa wana wa Manase;

55matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;

56na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;

57na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

58na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

59tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Gamalieli mwana wa Pedasuri.

60Siku ya kenda Abidani mwana wa Gideoni, mkuu wa wana wa Benyamini;

61matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;

62na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;

63na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

64na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

65tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Abidani mwana wa Gideoni.

66Siku ya kumi Ahiezeri mwana wa Amishadai, mkuu wa wana wa Dani;

67matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;

68na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;

69na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

70na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

71tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Ahiezeri mwana wa Amishadai.

72Na siku ya kumi na moja Pagieli mwana wa Okrani, mkuu wa wana wa Asheri;

73matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;

74na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;

75na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

76na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

77tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Pagieli mwana wa Okrani.

78Na siku ya kumi na mbili Ahira mwana wa Enani, mkuu wa wana wa Naftali;

79matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;

80na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;

81na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

82na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

83tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Ahira mwana wa Enani.

84Hayo ndiyo matoleo yaliyotolewa na wakuu wa Israeli kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, siku hiyo ilipotiwa mafuta; sahani za fedha kumi na mbili, na bakuli za fedha kumi na mbili, na vijiko vya dhahabu kumi na viwili;

85kila sahani ya fedha uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na kila bakuli uzani wake ni shekeli sabini; fedha yote ya vile vyombo ilikuwa shekeli elfu mbili na mia nne, kwa shekeli ya mahali patakatifu;

86na vijiko vya dhahabu vilivyojaa uvumba kumi na viwili, uzani wake kila kijiko shekeli kumi, kwa shekeli ya mahali patakatifu; dhahabu yote ya vile vijiko ilikuwa shekeli mia na ishirini;

87ng'ombe wote waliokuwa wa sadaka ya kuteketezwa walikuwa ng'ombe waume kumi na wawili, na hao kondoo waume walikuwa kumi na wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza walikuwa kumi na wawili, pamoja na sadaka yao ya unga; na mbuzi waume wa sadaka ya dhambi ni kumi na wawili;

88na ng'ombe wote waliokuwa wa dhabihu ya sadaka za amani ni ng'ombe waume ishirini na wanne, na hao kondoo waume walikuwa ni sitini, na hao mbuzi waume walikuwa ni sitini, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza walikuwa sitini. Hayo ndiyo matoleo yaliyotolewa kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, baada ya hiyo madhabahu kutiwa mafuta.

89Kisha, Musa alipoingia ndani ya hema ya kukutania ili kunena na Mungu ndipo alipoisikia Sauti ikinena naye kutoka hapo juu ya kiti cha rehema, kilichokuwa juu ya sanduku la ushahidi, ikitoka kati ya yale makerubi mawili; naye akanena naye.