Zaburi - Sura ya 105

Zaburi - Sura ya 105

1Haleluya.

2Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi, Zitafakarini ajabu zake zote.

3Jisifuni kwa jina lake takatifu, Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.

4Mtakeni Bwana na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote.

5Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya, Miujiza yake na hukumu za kinywa chake.

6Enyi wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake; Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.

7Yeye, Bwana, ndiye Mungu wetu; Duniani mwote mna hukumu zake.

8Analikumbuka agano lake milele; Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.

9Agano alilofanya na Ibrahimu, Na uapo wake kwa Isaka.

10Alilomthibitishia Yakobo liwe amri, Na Israeli liwe agano la milele.

11Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani, Iwe urithi wenu mliopimiwa.

12Walipokuwa watu wawezao kuhesabiwa, Naam, watu wachache na wageni ndani yake,

13Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa, Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine.

14Hakumwacha mtu awaonee, Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao.

15Akisema, Msiwaguse masihi

16Akaiita njaa iijilie nchi, Akakiharibu chakula chote walichokitegemea.

17Alimpeleka mtu mbele yao, Yusufu aliuzwa utumwani.

18Walimwumiza miguu yake kwa pingu, Akatiwa katika minyororo ya chuma.

19Hata wakati wa kuwadia neno lake, Ahadi ya Bwana ilimjaribu.

20Mfalme alituma watu akamfungua, Mkuu wa watu akamwachia.

21Akamweka kuwa bwana wa nyumba yake, Na mwenye amri juu ya mali zake zote.

22Awafunge masheki wake kama apendavyo, Na kuwafundisha wazee wake hekima.

23Israeli naye akaingia Misri, Yakobo akawa mgeni katika nchi ya Hamu.

24Akawajalia watu wake wazae sana, Akawafanya kuwa hodari kuliko watesi wao.

25Akawageuza moyo wawachukie watu wake, Wakawatendea hila watumishi wake.

26Akamtuma Musa, mtumishi wake, Na Haruni ambaye amemchagua.

27Akaweka mambo ya ishara zake kati yao, Na miujiza katika nchi ya Hamu.

28Alituma giza, kukafunga giza, Wala hawakuyaasi maneno yake.

29Aliyageuza maji yao yakawa damu, Akawafisha samaki wao.

30Nchi yao ilijaa vyura, Vyumbani mwa wafalme wao.

31Alisema, kukaja makundi ya mainzi, Na chawa mipakani mwao mwote.

32Badala ya mvua aliwapa mvua ya mawe, Na moto wa miali katika nchi yao.

33Akaipiga mizabibu yao na mitini yao, Akaivunja miti ya mipaka yao.

34Alisema, kukaja nzige, Na tunutu wasiohesabika;

35Wakaila miche yote ya nchi yao, Wakayala matunda ya ardhi yao.

36Akawapiga wazaliwa wa kwanza katika nchi, Malimbuko ya nguvu zao.

37Akawatoa hali wana fedha na dhahabu, Katika kabila zao asiwepo mwenye kukwaa.

38Misri ilifurahi walipoondoka, Maana kwa ajili yao hofu imewaangukia.

39Alitandaza wingu liwe funiko, Na moto utoe nuru usiku.

40Walipotaka akaleta kware, Akawashibisha chakula cha mbinguni.

41Akaufunua mwamba, kukabubujika maji, Yakapita pakavuni kama mto.

42Maana alilikumbuka neno lake takatifu, Na Ibrahimu, mtumishi wake.

43Akawatoa watu wake kwa shangwe, Na wateule wake kwa nyimbo za furaha.

44Akawapa nchi za mataifa, wakairithi kazi ya watu;

45Ili wazishike amri zake, na kuzitii sheria zake. Haleluya.