Zaburi - Sura ya 113

Zaburi - Sura ya 113

1Haleluya. Enyi watumishi wa Bwana, sifuni, Lisifuni jina la Bwana.

2Jina la Bwana lihimidiwe Tangu leo na hata milele.

3Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la Bwana husifiwa.

4Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote, Na utukufu wake ni juu ya mbingu.

5Ni nani aliye mfano wa Bwana, Mungu wetu aketiye juu;

6Anyenyekeaye kutazama, Mbinguni na duniani?

7Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani.

8Amketishe pamoja na wakuu, Pamoja na wakuu wa watu wake.

9Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha.