Zaburi - Sura ya 114

1Haleluya. Israeli alipotoka Misri, Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni.
2Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake.
3Bahari iliona ikakimbia, Yordani ilirudishwa nyuma.
4Milima iliruka kama kondoo waume, Vilima kama wana-kondoo.
5Ee bahari, una nini, ukimbie? Yordani, urudi nyuma?
6Enyi milima, mruke kama kondoo waume? Enyi vilima, kama wana-kondoo?
7Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana, Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo.
8Augeuza mwamba kuwa ziwa la maji, Jiwe gumu kuwa chemchemi.