Zaburi - Sura ya 117

Zaburi - Sura ya 117

1Haleluya. Enyi mataifa yote, msifuni Bwana, Enyi watu wote, mhimidini.

2Maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu, Na uaminifu wa Bwana ni wa milele.