Zaburi - Sura ya 12

Zaburi - Sura ya 12

1Bwana, uokoe, maana mcha Mungu amekoma, Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu.

2Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki;

3Bwana ataikata midomo yote ya kujipendekeza, Nao ulimi unenao maneno ya kiburi;

4Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda; Midomo yetu ni yetu wenyewe, Ni nani aliye bwana juu yetu?

5Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema Bwana, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.

6Maneno ya Bwana ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.

7Wewe, Bwana, ndiwe utakayetuhifadhi, Utatulinda na kizazi hiki milele.

8Wasio haki hutembea pande zote, Ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu.