Zaburi - Sura ya 121

1Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi?
2Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.
3Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye;
4Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume.
6Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku.
7Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako.
8Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.