Zaburi - Sura ya 122

Zaburi - Sura ya 122

1Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana.

2Miguu yetu imesimama Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu.

3Ee Yerusalemu uliyejengwa Kama mji ulioshikamana,

4Huko ndiko walikopanda kabila, Kabila za Bwana; Ushuhuda kwa Israeli, Walishukuru jina la Bwana.

5Maana huko viliwekwa viti vya hukumu, Viti vya enzi vya mbari ya Daudi.

6Utakieni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao;

7Amani na ikae ndani ya kuta zako, Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.

8Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu Niseme sasa, Amani ikae nawe.

9Kwa ajili ya nyumba ya Bwana, Mungu wetu, Nikutafutie mema.