Zaburi - Sura ya 123

1Nimekuinulia macho yangu, Wewe uketiye mbinguni.
2Kama vile macho ya watumishi Kwa mkono wa bwana zao Kama macho ya mjakazi Kwa mkono wa bibi yake; Hivyo macho yetu humwelekea Bwana, Mungu wetu, Hata atakapoturehemu.
3Uturehemu, Ee Bwana, uturehemu sisi, Kwa maana tumeshiba dharau.
4Nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha, Na dharau ya wenye kiburi.