Zaburi - Sura ya 124

Zaburi - Sura ya 124

1Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa,

2Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Wanadamu walipotushambulia.

3Papo hapo wangalitumeza hai, Hasira yao ilipowaka juu yetu

4Papo hapo maji yangalitugharikisha, Mto ungalipita juu ya roho zetu;

5Papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetu Maji yafurikayo.

6Na ahimidiwe Bwana; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao.

7Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka.

8Msaada wetu u katika jina la Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.