Zaburi - Sura ya 125

Zaburi - Sura ya 125

1Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.

2Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele.

3Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki; Wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu.

4Ee Bwana, uwatendee mema walio wema, Nao walio wanyofu wa moyo.

5Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, Bwana atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.