Zaburi - Sura ya 126

Zaburi - Sura ya 126

1Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto.

2Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, Bwana amewatendea mambo makuu.

3Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi.

4Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini.

5Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.

6Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.