Zaburi - Sura ya 128

Zaburi - Sura ya 128

1Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake.

2Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.

3Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Vyumbani mwa nyumba yako. Wanao kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako.

4Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana.

5Bwana akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;

6Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.