Zaburi - Sura ya 129

Zaburi - Sura ya 129

1Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Israeli na aseme sasa,

2Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Lakini hawakuniweza.

3Wakulima wamelima mgongoni mwangu, Wamefanya mirefu mifuo yao.

4Bwana ndiye mwenye haki, Amezikata kamba zao wasio haki.

5Na waaibishwe, warudishwe nyuma, Wote wanaoichukia Sayuni.

6Na wawe kama majani ya darini Yanyaukayo kabla hayajamea.

7Ambayo mvunaji haujazi mkono wake, Wala mfunga miganda kifua chake.

8Wala hawasemi wapitao, Amani ya Bwana ikae nanyi, Twawabariki kwa jina la Bwana.