Zaburi - Sura ya 13

Zaburi - Sura ya 13

1Ee Bwana, hata lini utanisahau, hata milele? Hata lini utanificha uso wako?

2Hata lini nifanye mashauri nafsini mwangu, Nikihuzunika moyoni mchana kutwa? Hata lini adui yangu atukuke juu yangu?

3Ee Bwana, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti.

4Adui yangu asije akasema, Nimemshinda; Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa.

5Nami nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.

6Naam, nimwimbie Bwana, Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.