Zaburi - Sura ya 130

 Zaburi - Sura ya 130

1Ee Bwana, toka vilindini nimekulilia.

2Bwana, uisikie sauti yangu. Masikio yako na yaisikilize Sauti ya dua zangu.

3Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama?

4Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe.

5Nimemngoja Bwana, roho yangu imengoja, Na neno lake nimelitumainia.

6Nafsi yangu inamngoja Bwana, Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, Naam, walinzi waingojao asubuhi.

7Ee Israeli, umtarajie Bwana; Maana kwa Bwana kuna fadhili, Na kwake kuna ukombozi mwingi.

8Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote.