Zaburi - Sura ya 133

Zaburi - Sura ya 133

1Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja.

2Ni kama mafuta mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.

3Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko Bwana alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele.