Zaburi - Sura ya 134

Zaburi - Sura ya 134

1Tazama, enyi watumishi wa Bwana, Mhimidini Bwana, nyote pia. Ninyi mnaosimama usiku Katika nyumba ya Bwana.

2Painulieni patakatifu mikono yenu, Na kumhimidi Bwana.

3Bwana akubariki toka Sayuni, Aliyezifanya mbingu na nchi.