Zaburi - Sura ya 136

Zaburi - Sura ya 136

1Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

2Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

3Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

4Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

5Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

6Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

7Yeye aliyefanya mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

8Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

9Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

10Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

11Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

12Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

13Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

14Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

15Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

16Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

17Yeye aliyewapiga wafalme wakuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

18Akawaua wafalme mashuhuri; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

19Sihoni, mfalme wa Waamori; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

20Na Ogu, mfalme wa Bashani; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

21Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

22Urithi wa Israeli mtumishi wake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

23Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

24Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

25Kila chenye mwili akipa chakula chake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

26Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.