Zaburi - Sura ya 137

1Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni.
2Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu.
3Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni.
4Tuuimbeje wimbo wa Bwana Katika nchi ya ugeni?
5Ee Yerusalemu, nikikusahau wewe, Mkono wangu wa kuume na usahau.
6Ulimi wangu na ugandamane Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka. Nisipoikuza Yerusalemu Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu.
7Ee Bwana, uwakumbuke wana wa Edomu, Siku ya Yerusalemu. Waliosema, Bomoeni! Bomoeni hata misingini!
8Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia, Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi.
9Heri yeye atakayewakamata wadogo wako, Na kuwaseta wao juu ya mwamba.