Zaburi - Sura ya 146

Zaburi - Sura ya 146

1Haleluya.

2Nitamsifu Bwana muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.

3Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.

4Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.

5Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, Na tumaini lake ni kwa Bwana, Mungu wake,

6Aliyezifanya mbingu na nchi, Bahari na vitu vyote vilivyomo. Huishika kweli milele,

7Huwafanyia hukumu walioonewa, Huwapa wenye njaa chakula; Bwana hufungua waliofungwa;

8Bwana huwafumbua macho waliopofuka; Bwana huwainua walioinama; Bwana huwapenda wenye haki;

9Bwana huwahifadhi wageni; Huwategemeza yatima na mjane; Bali njia ya wasio haki huipotosha.

10Bwana atamiliki milele, Mungu wako, Ee Sayuni, kizazi hata kizazi. Haleluya.