Zaburi - Sura ya 149

1Haleluya. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Sifa zake katika kusanyiko la watauwa.
2Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya, Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.
3Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa matari na kinubi wamwimbie.
4Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu.
5Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.
6Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao, Na upanga mkali kuwili mikononi mwao.
7Ili kufanya kisasi juu ya mataifa, Na adhabu juu ya kabila za watu.
8Wawafunge wafalme wao kwa minyororo, Na wakuu wao kwa pingu za chuma.
9Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa; Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote. Haleluya.