Zaburi - Sura ya 16

Zaburi - Sura ya 16

1Mungu, unihifadhi mimi, Kwa maana nakukimbilia Wewe.

2Nimemwambia Bwana, Ndiwe Bwana wangu; Sina wema ila utokao kwako.

3Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.

4Huzuni zao zitaongezeka Wambadilio Mungu kwa mwingine; Sitazimimina sadaka zao za damu, Wala kuyataja majina yao midomoni mwangu.

5Bwana ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe changu; Wewe unaishika kura yangu.

6Kamba zangu zimeniangukia mahali pema, Naam, nimepata urithi mzuri.

7Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri, Naam, mtima wangu umenifundisha usiku.

8Nimemweka Bwana mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.

9Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nao utukufu wangu unashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.

10Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.

11Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.