Zaburi - Sura ya 20

Zaburi - Sura ya 20

1Bwana akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.

2Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni.

3Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako.

4Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote.

5Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. Bwana akutimizie matakwa yako yote.

6Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi

7Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu.

8Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama.

9Bwana, umwokoe mfalme, Utuitikie siku tuitayo.