Zaburi - Sura ya 29

1Mpeni Bwana, enyi wana wa Mungu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu;
2Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu.
3Sauti ya Bwana i juu ya maji; Mungu wa utukufu alipiga radi; Bwana yu juu ya maji mengi.
4Sauti ya Bwana ina nguvu; Sauti ya Bwana ina adhama;
5Sauti ya Bwana yaivunja mierezi; Naam, Bwana aivunja-vunja mierezi ya Lebanoni;
6Airusha-rusha kama ndama wa ng'ombe; Lebanoni na Sirioni kama mwana-nyati.
7Sauti ya Bwana yaipasua miali ya moto;
8Sauti ya Bwana yalitetemesha jangwa; Bwana alitetemesha jangwa la Kadeshi.
9Sauti ya Bwana yawazalisha ayala, Na kuifichua misitu; Na ndani ya hekalu lake Wanasema wote, Utukufu.
10Bwana aliketi juu ya Gharika; Naam, Bwana ameketi hali ya mfalme milele.
11Bwana atawapa watu wake nguvu; Bwana atawabariki watu wake kwa amani.