Zaburi - Sura ya 3
1Bwana, watesi wangu wamezidi kuwa wengi, Ni wengi wanaonishambulia,
2Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu.
3Na Wewe, Bwana, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.
4Kwa sauti yangu namwita Bwana Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.
5Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa Bwana ananitegemeza.
6Sitayaogopa makumi elfu ya watu, Waliojipanga juu yangu pande zote.
7Bwana, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki.
8Wokovu una Bwana; Baraka yako na iwe juu ya watu wako.