Zaburi - Sura ya 48
1Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu.
2Kuinuka kwake ni mzuri sana, Ni furaha ya dunia yote. Mlima Sayuni pande za kaskazini, Mji wa Mfalme mkuu.
3Mungu katika majumba yake Amejijulisha kuwa ngome.
4Maana, tazama, wafalme walikusanyika; Walipita wote pamoja.
5Waliona, mara wakashangaa; Wakafadhaika na kukimbia.
6Papo hapo tetemeko liliwashika, Utungu kama wa mwanamke azaaye.
7Kwa upepo wa mashariki Wavunja jahazi za Tarshishi.
8Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona, Katika mji wa Bwana wa majeshi. Mji wa Mungu wetu; Mungu ataufanya imara hata milele.
9Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu, Katikati ya hekalu lako.
10Kama lilivyo jina lako, Ee Mungu, Ndivyo na sifa yako hata miisho ya dunia. Mkono wako wa kuume umejaa haki;
11Na ufurahi mlima Sayuni. Binti za Yuda na washangilie Kwa sababu ya hukumu zako.
12Tembeeni katika Sayuni, Uzungukeni mji, Ihesabuni minara yake,
13Tieni moyoni boma zake, Yafikirini majumba yake, Mpate kuwaambia kizazi kitakachokuja.
14Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele Yeye ndiye atakayetuongoza.

Swahili
Italiano (it-IT)
Português do Brasil (pt-BR)
Polski (PL)
Deutsch (Deutschland)
Français (France)
Español (España)
Українська Біблія у перекладі Огієнка
English Bible - 21ST CENTURY KING JAMES (KJ21)