Zaburi - Sura ya 52

Zaburi - Sura ya 52

1Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote.

2Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila

3Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli.

4Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila.

5Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung'oa katika nchi ya walio hai.

6Nao wenye haki wataona; Wataingiwa na hofu na kumcheka;

7Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kujifanya hodari kwa madhara yake.

8Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.

9Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako.