Zaburi - Sura ya 54

1Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe, Na kwa uweza wako unifanyie hukumu.
2Ee Mungu, uyasikie maombi yangu, Uyasikilize maneno ya kinywa changu.
3Kwa maana wageni wamenishambulia; Watu watishao wananitafuta nafsi yangu; Hawakumweka Mungu mbele yao.
4Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia; Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu.
5Atawarudishia adui zangu ubaya wao; Uwaangamize kwa uaminifu wako.
6Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu; Ee Bwana, nitalishukuru jina lako, maana ni jema.
7Kwa kuwa limeniokoa na kila taabu; Na jicho langu limeridhika Kwa kuwatazama adui zangu.