Zaburi - Sura ya 63
1Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.
2Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, Nizione nguvu zako na utukufu wako.
3Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu.
4Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
5Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
6Ninapokukumbuka kitandani mwangu, Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku.
7Maana Wewe umekuwa msaada wangu, Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.
8Nafsi yangu inakuandama sana; Mkono wako wa kuume unanitegemeza.
9Bali waitafutao nafsi yangu, ili kuiharibu, Wataingia pande za nchi zilizo chini.
10Watatolewa wafe kwa nguvu za upanga, Watakuwa riziki za mbwa-mwitu.
11Bali mfalme atamfurahia Mungu, Kila aapaye kwa Yeye atashangilia, Kwa maana vinywa vya waongo vitafumbwa.

Swahili
Italiano (it-IT)
Português do Brasil (pt-BR)
Polski (PL)
Deutsch (Deutschland)
Français (France)
Español (España)
Українська Біблія у перекладі Огієнка
English Bible - 21ST CENTURY KING JAMES (KJ21)