Zaburi - Sura ya 67

Zaburi - Sura ya 67

1Mungu na atufadhili na kutubariki, Na kutuangazia uso wake.

2Njia yake ijulike duniani, Wokovu wake katikati ya mataifa yote.

3Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru.

4Mataifa na washangilie, Naam, waimbe kwa furaha, Maana kwa haki utawahukumu watu, Na kuwaongoza mataifa walioko duniani.

5Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru.

6Nchi imetoa mazao yake MUNGU, Mungu wetu, ametubariki.

7Mungu atatubariki sisi; Miisho yote ya dunia itamcha Yeye.