Zaburi - Sura ya 70

Zaburi - Sura ya 70

1Ee Mungu, uniokoe, Ee Bwana, unisaidie hima.

2Waaibike, wafedheheke, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu.

3Warudi nyuma, na iwe aibu yao, Wanaosema, Ewe! Ewe!

4Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu.

5Nami ni maskini na mhitaji, Ee Mungu, unijilie kwa haraka. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Bwana, usikawie.