Zaburi - Sura ya 8

Zaburi - Sura ya 8

1Wewe, MUNGU, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni;

2Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe; Uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi.

3Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha;

4Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?

5Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;

6Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.

7Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni;

8Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.

9Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!