Zaburi - Sura ya 82

Zaburi - Sura ya 82

1Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu; Katikati ya miungu anahukumu.

2Hata lini mtahukumu kwa dhuluma, Na kuzikubali nyuso za wabaya?

3Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa na fukara;

4Mwokoeni maskini na mhitaji; Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.

5Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; Misingi yote ya nchi imetikisika.

6Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia.

7Lakini mtakufa kama wanadamu, Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.

8Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi, Maana Wewe utawarithi mataifa yote.