Zaburi - Sura ya 87

Zaburi - Sura ya 87

1Msingi wake upo Juu ya milima mitakatifu.

2Bwana ayapenda malango ya Sayuni Kuliko maskani zote za Yakobo.

3Umetajwa kwa mambo matukufu, Ee Mji wa Mungu.

4Nitataja Rahabu na Babeli Miongoni mwao wanaonijua. Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi; Huyu alizaliwa humo.

5Naam, mintarafu Sayuni itasemwa, Huyu na huyu alizaliwa humo. Na Yeye Aliye juu Ataufanya imara.

6Bwana atahesabu, awaandikapo mataifa, Huyu alizaliwa humo.

7Waimbao na wachezao na waseme, Visima vyangu vyote vimo mwako.