Zaburi - Sura ya 93

Zaburi - Sura ya 93

1Bwana ametamalaki, amejivika adhama, Bwana amejivika, na kujikaza nguvu. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;

2Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani; Wewe ndiwe uliye tangu milele.

3Ee Bwana, mito imepaza, Mito imepaza sauti zake, Mito imepaza uvumi wake.

4Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu, Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo, Bwana Aliye juu ndiye mwenye ukuu.

5Shuhuda zako ni amini sana; Utakatifu ndio uifaao nyumba yako, Ee Bwana, milele na milele.